BANGI YAPIKIWA KWENYE MBOGA MKOANI GEITA.
Kuanzishwa kwa operesheni maalumu ya kudhibiti
biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini baadhi ya wavuvi wa samaki
katika Ziwa Victoria wamebuni mbinu mpya ya utumiaji wa dawa za kulevya kwa
kupika bangi kwenye mboga ya samaki wakihofia kukamatwa hali inayohatalisha
maisha ya watu watakaokula chakula bila kufahamu.
Uchunguzi umebaini
baadhi ya wavuvi wa samaki katika Ziwa Victoria wamebadilisha matumizi ya dawa
za kulevya aina ya bangi kwa kuipika kwenye mboga ya samaki ambapo mmoja wa
wazee wanaoishi kando kando ya Ziwa Victoria ameeleza kuwa kumekuwa na tabia
hiyo ambayo ni hatarishi.
Baadhi ya wazee wa wilaya ya Chato mkoani Geita
wameipongeza serikali kwa kudhibiti usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya
hapa nchini ambao umeathiri nguvu kazi ya taifa.
Post a Comment