Header Ads

JERUSALEM STUDIO MKOMBOZI KWA JAMII YA WASANII GEITA.

Meneja wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya BRIGHT LIGHT ORGANIZATION na mkurugenzi wa Jerusalem Studio Bwana KENETH SIMON SINDILO,ameamua kubadili matumizi ya nyumba iliyokuwa ikijengwa kwa lengo la kuishi kuwa Ofisi na Studio ya kurekodia ambayo ni nzuri na ni ya kisasa iliyopewa jina la JERUSALEM STUDIO.

Akiongea na blog hii Sindilo amesema alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na baadhi ya wataalam wa muziki.Hadi sasa Studio hiyo tayari imekamilika na iko kwenye hatua za mwisho za marekebisho madogo madogo ili kuifanya iwe si tu Studio kwa ajili ya wasanii na waimbaji wa Geita bali Afrika mashariki.
Amewasihi waimbaji wote wakiwemo wakiwemo wa Injili,Bongo fleva na wengine kuja kurekodi katika studio hii kwani kuna wataalamu wa kila aina na vyombo vya kisasa.

Pia waweza kuwasiliana moja kwa moja na uongozi wa studio hiyo kwa simu namba 0767 262 583


                                            Mwonekano wa jengo la studio ya Jerusalem





















                          Producer akiwa anaangalia kitu akiwa ndani ya Studio za Jerusalem.

mwonekano wa studio kwa ndani



Mkurugenzi JERUSALEM STUDIO Bw.Keneth Sindilo.





























No comments