Header Ads

WAMBURA MTANI WA RFA AZIMA SIMU KWA MADENI.



Ukitaja jina la WAMBURA MTANI bila shaka si geni masikioni mwa WATANZANIA walio wengi na hii ni kutokana na umaarufu wa kipindi chake cha JE,HUU NI UUNGWANA? Kinachorushwa kupitia RFA kila Jumapili saa tatu asubuhi.
Wambura amemaliza mwaka 2016 kwa lawama ya kutolipa deni analodaiwa na mwandishi na ripota wa STARTV mkoani Geita SALMA MRISHO ambalo hata hivyo haikuwekwa wazi ni kiasi gani cha pesa Wambura anadaiwa.
Kupitia akaunti yake ya facebook tarehe 31/12/2016 saa 10:02 jioni Salma aliandika"Mwaka 2016 unaishia ikimpendeza mungu tutauona mwaka 2017 nashkuru kwa wale wote  niliowakopesha hela ambao hata simu zangu hawapokei kwa sasa kama Wambura Mtani wengine nawastahi kwa vile mnapokeaga simu zangu na wale waliotaka kunitumbua mwaka 2016 wakina Barongo kwa uwezo wa Mungu amenipigania bado napumua."

Jambo hilo lilionekana kuwashangaza baadhi ya watu kutokana na sifa ya nguli huyo wa habari kurekebisha tabia za watu na kujisahau hadi kufanya hivyo.


Mwaka 2016 unaishia ikimpendeza mungu tutauona mwaka 2017 nashkuru kwa wale wote wale wote niliowakopesha hela ambao hata simu zangu hawapokei kwa sasa kama Wambura Mtani wengine nawastahi kwa vile mnapokeaga simu zangu na wale waliotaka kunitumbua mwaka 2016 wakina Barongo kwa uwezo wa Mungu amenipigania bado napumua.
Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya Inshaalah panapo majaliwa tutakutana hapa hapa FB.

No comments