VINYAGO VYA SHULE VYAZUA MVUTANO MKALI GEITA.
Serikali Mkoani
Geita,imeendelea kusisitiza kuwa itatoa
zawadi kwa shule ambazo zitafanya vizuri na zile ambazo zitafanya vibaya
zitapatiwa zawadi ya vinyago hivyo walimu wametakiwa kufundisha kwa bidii ,na
kuweka malengo ya ufaulu ili kuepukana na zawadi hiyo ambayo itatolewa kwa shule ambayo itafanya
vibaya kwenye mitihani ya kitaifa.
Kauli hiyo
imetolewa na Afisa Elimu mkoa wa Geita Bi.Rehema Mbwilo ambaye pia ni katibu
tawala msaidizi wa mkoa alipotembelewa
ofisini kwake na Blog hii kutaka kujua juu ya kauli aliyowahi kuitoa mwezi
desemba mwaka jana wakati wa kutangaza matokeo ya darasa la saba na kuiagiza
halmashauri kutaandaa vinyago vitakavyowekwa
kwenye meza za wakuu wa shule ambao shule zao zimefanya vibaya.
“Tunafanya hivi ili kuweza ku maintain status ya mkoa na
kumfanya kila mwalimu awajibike hasahasa masomo ya sekondari ambayo kila mwalimu
ana specialization yake” amesema Mbwilo.
” Sisi walimu tunapokuwa chuoni tuna aina mbili za zawadi
ambazo mwanafunzi unayemfundisha darasani lazima apewe,tuna zawadi chanya na
zawadi hasi….zawadi hasi ina mpa changamoto huyu aliyefanya vibaya kuongeza
bidii ili aweze kufanya vizuri”Ameongeza
“La msingi walimu wafanye kazi kwa bidii ili waepukane na
zawadi hasi….zawadi hizi zote mbili tutazitoa kwa walimu pamoja na maafisa
elimu” Alisisitiza Bi. Rehema Mbwilo.
Kwa upande
wake kaimu katibu wa chama cha walimu mkoa wa Geita Mwl.John Kafimbi amelaani
vikali kauli hiyo ya afisa elimu na kusema kuwa inadhoofisha utendaji kazi wa
walimu kwani utaratibu huo unamdhalilisha mwalimu.
Kafimbi
ameongeza kuwa vinyago hivyo kwanza vitapoteza pesa ambazo zingefanya mambo ya
maana,ameitaka serikali ya mkoa ishughulikie changamoto za uhaba wa
madawati,vyumba vya madarasa,nyumba za walimu pamoja na madeni wanayodai walimu
badala ya kuwaza kutengeneza vinyago.
Post a Comment