Header Ads

RAIS MAGUFULI AGONGELEA MSUMARI MSIMAMO WA KUTOTOA CHAKULA.


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada huku akiwahimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame ili kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha masanza kona wilayani busega mara baada ya kuwasili akitokea mkoani mwanza Rais Magufuli amewashukuru wananchi kwa kumchagua oktoba 25 mwaka 2015 na kuahidi kutatua matatizo yanayowakabili yakiwemo ya maji na umeme .

Aidha amesisitiza kutotoa chakula cha msaada kwa wananchi na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii sambamba na kulima mazao yanayostahimili ukame kama vile mtama ,viazi na ufuta.

Rais magufuli ameahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha kilomita 50 kwa kiwango cha lami kutoka Bariadi mjini hadi Maswa baada ya kukamilika kwa barabara ya Lamadi Bariadi yenye urefu wa km 72.8.

pom3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Magu mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
pom4 pom5 pom6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

No comments