Header Ads

Kisonono sugu chaibuka upya Uingereza.


Image copyrightThinkstock
Image captionUgonjwa huo hausikii dawa aina ya azithromycin na ceftriaxone.

Kisonono kinaweza kuwa moja ya magonjwa sugu, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza ameonya.
Bi Sally Davies ameandikia waganga wote na maduka ya dawa ili kuhakikisha kuwa wanatoa maagizo na dawa sahihi baada ya kupatikana kwa " kisonono sugu " katika mji wa Leeds.
Onyo hilo linakuja baada ya wasiwasi kuongezeka kufuatia habari kuwa baadhi ya wagonjwa walikuwa hawapati matibabu kamili na dawa za kutosha zinazohitajika kumaliza kikamilifu maambukizi ya kisonono.
Madaktari wa afya ya uzazi na kijinsia wanasema kuwa kisonono kinazidi kuwa sugu.
Watu wenye ugonjwa sugu wa kisonono waligundulika kaskazini mwa Uingereza mwezi Machi.
Ugonjwa huo hausikii dawa aina ya azithromycin na ceftriaxone.
Katika barua yake, afisa huyo mkuu wa matibabu alisema: "Kisonono iko katika hatari ya kuwa sugu''
Awali wagonjwa wenye kisonono walikuwa wanatibiwa kwa sindano ya ceftriaxone na kidonge cha azithromycin hata hivyo baadhi ya wagonjwa wameanza kuonekana kutosikia mchanganyiko huo wa dawa''.

Image copyrightSPL
Image captionKisonono sugu chaibuka upya Uingereza

Mapema mwaka huu, Shirika la Uingereza la Afya ya Uzazi na HIV (BASHH) alionya kuwa baadhi ya maduka ya dawa yalikuwa yanatoa vidonge tu kwa watgonjwa wenye kisonono badala ya kutoa matibabu ya sindano na vidonge.
Kutumia moja tu ya dawa mbili inafanya kuwa rahisi kwa bakteria kuendeleza upinzani.
Barua, ambayo pia imewekwa saini na afisa mkuu wa dawa Dakta Keith Ridge, alisema: "Kisonono hainabudi kukabiliwa kwa haraka ilikumaliza uwezo wa ke kuwa sugu''
CHANZO:BBC SWAHILI

No comments