Wanafunzi waandamana Washington DC
Karibu wanafunzi 1,000 wa shule za sekondari kutoka Washington DC, na maeneo ya jirani walitoka mashuleni na kuandamana kuzunguka mjini hapo Jumanne, wakimpinga rais mteule wa Marekani, Donald Trump.
Kwa mujibu wa mwanafunzi mmoja aliyeongea na VOA alisema kwamba klabu ya haki za binadamu katika shule ya Wilson iliyopo Washington,ilipanga maandamano hayo.
Amesema klabu hiyo iliwafahamisha wanafunzi kupitia mitandao ya kijamii na kuwaandikia wazazi kupitia barua pepe nia yao ya kupanga kutoka mashuleni na kuandamana katikati ya mji hapo jana.
Licha ya kwamba mamia ya wanafunzi hao hawakupiga kura, walitaka kutoa maoni yao kuhusu rais mteule na wasiwasi wao kuhusu mustakabali wao wa baadaye.
Source:VOA

Post a Comment