Header Ads

Upelelezi wa Kesi ya Scorpion Wakamilika, Kuanza Kusikilizwa Novemba 30

Dar es Salaam: Upelelezi wa kesi ya kudaiwa kumtoboa macho, kumjeruhi tumboni na kumpora fedha na mkufu Said Mrisho inayomkabili mkazi wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion umekamilika na kesi inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 30, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na hakimu Flora Lymo anayesikiliza kesi hiyo. Scorpion aliomba asomewe maelezo ya awali lakini hakimu alikataa. Ulinzi ulikuwa mkali muda wote.

Source: Global Publisher

No comments