Header Ads

Meli ya mizigo yazama Bahari ya Hindi


MELI ya Mizigo ya Mv. Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda  Zanzibar  imezama katika Bahari ya Hindi ikiwa imebeba mbao zaidi ya 1090 na magunia 450 ya viazi mviringo.
 
Hata hivyo,  mabaharia 12 ambao ni wafanyakazi katika meli ya mizigo  ya hiyo wamesalimika kufa maji  kwa vile meli hiyo  haikuzama yote  katika eneo la Kizingo  kisiwani Zanzibar.
 
Tukio hilo lilitokea jana alfajiri kisiwani Unguja. Mkuu wa Operesheni baharini, Msilimiwa Idd,  alisema tukio hilo lilitokea saa 8.00 usiku baada ya meli hiyo kuyumba kutokana na dhoruba kali ya upepo.
 
Alisema ilipotimu saa saa 9.00usiku nahodha wa meli hiyo alipoona hali imezidi kuwa mbaya akaelekea katika Kisiwa Mchanga  ambako alijikuta akikwama kwa vile upande mmoja wa meli ulikuwa unapitisha maji.

No comments