Waziri Mwakyembe kulishitaki gazeti la Dira lililosema ametapeli bilioni 2
June 21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe alikanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi.
"Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu " Amesem a waziri Mwakyembe na kuongeza
"Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji
"Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema kifaru chake cha kivita kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na kulitia doa jeshi letu. Tukikaa kimya tutaambiwa tena kuwa hicho kifaru kinatumika kama daladala.
"Tutafungua kesi hii mahakama kuu ya Tanzania na bado mimi na mawakili wangu tunaangalia impact na kuhusika kwa vyombo vikubwa vya habari kama ITV na Star Tv kwa kutangaza taarifa "
Post a Comment