Serikali Yafika Eneo L a Mgusu Walipokufa Wachimbaji Kwa Kufukiwa na Kifusi
Kamati ya Ulinzi na Usalama Ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa walipotembelea Mtaa wa Mgusu ambapo machi tisa Wachimbaji Watano walifukiwa na kifusi na kufariki huku watatu wakijeruhiwa.
Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwassa akiangalia eneo la tukio.
Nae Naibu Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani aliwasili eneo lililotokea tukio na kuzungumza na Wachimbaji Wadogo na kuwataka kuwa wavumilivu kwani machimbo hayo yanafungwa kwa muda ambapo yatafanyiwa marekebisho ili wachimbaji hao wachimbe mahali salama.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani akizungumza na Wachimbaji Wadogo eneo la Mgusu.
PICHA,HABARI:GEITA INFO (Salma Mrisho)
Post a Comment