SAMATTA AWEKA REKODI MPYA GENK
Mbwana Samatta ameendelea kufanya yale ambayo watanzania wengi wamekuwa wakisubi kwa hamu kutoka kwa nyota huyo tangu alipojiunga na klabu ya Genk ya Belgium baada ya kufunga bao la kwanza wakati Genk inaitandika Oostende kwa magoli 4-1 kwenye ligi ya Belgium Pro Leaue.
Mbali na Samatta kufunga goli hilo, kija huyo ambaye anatokea maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam, alipewa fursa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza ikiwa ni mara yake ya kwanza kuanza kwenye kikosi cha kwanza tangu atue Genk.
Mara zote Samatta amekuwa akitokea benchi kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa kigiriki Nikolaos Karelis. Hilo ni goli la pili kwa Samatta akiwa na Genk baada ya kufunga bao lake la kwanza February 28 wakati timu yake ilipoifunga Club Brugge magoli 3-2.
Samatta anafanikiwa kuweka rekodi yake ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kufunga goli.
Post a Comment