Header Ads

MKUU WA WILAYA YA BUKOMBE ATAKIWA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI.


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Bukombe Mkoani Geita imemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Aman Mwenegoha afike mahakamani bila kukosa siku ya jumatatu machi,14,2016 saa 2.30 asubuhi.
Mwenegoha amepewa wito huo wa Mahakama ya wilaya  kufika ili kutoa ushahidi dhidi ya kesi inayomkabili Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja iliyoko kata ya Katente mjini ushirombo James Nying’ati aliyekamatwa akipokea Rushwa kutoka kwa Mzazi Marco Elias ili ampatie nafasi mtoto  wake arudie darasa la Saba.
Mkuu huyo wa Wilaya amekiri kupokea hati hiyo ya wito wa mahakama toka TAKUKURU na ameshasaini na siku hiyo atafika mahakamani hapo kutoa ushahidi.

Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Bukombe Chuzera Shija amethibitisha kuwa kweli mahakama imempelekea Mkuu wa Wilaya hati ya Wito(samansi) ili afike mahakama ya wilaya kutoa ushahidi huo. 
Hivi karibuni mwezi februari TAKUKURU iliweka mtego na kuweza kumkamata mwalimu huyo mkuu wa shule ya msingi Umoja James Nying’ati aliyeomba Rushwa toka kwa mzazi ili ampatie msaada wa mwanaye kurudia darasa la saba.
Shija ameionya jamii iache kabisa tabia za kutoa ,kuomba ama kupokea Rushwa ya aina yoyote. 

No comments