JELA MIAKA MINNE KWA WIZI WA PIKIPIKI.
NA MAKUNGA MAKUNGA,
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imewahukumu watu wanne kwenda kutumikia kifungo jela miaka minne kila mmoja kwa kosa la wizi wa Pikipiki aina ya SANLG.
Waliohukumiwa kifungo jera ni Marco Emanuel Teso mkazi wa Katoro na wenzake watatu ambao ni Elisha John naye ni makzi wa katoro geita na wengine ni Paskal Hamis mkazi wa katente na Nelson Mandela mkazi wa kapera mjini ushirombo.
Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Gabriel Kurwijila, mwendesha mashtaka wa Polisi Elias Mgobera ameiambia mahakama kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo julai 6 mwaka jana majira ya saa nane za usiku huko katika mtaa wa kapera masakuroni ambako walifanya njama na kuiba Pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajiri T192 ADL mali ya Andrew Jackson yenye thamani ya sh.1,790,000 .
Alisema Paskal Hamis ndiye aliyekuwa mwendesha Bodaboda hiyo aliyekuwa ameajiliwa na Andrew, usiku huo alitoka Wadutya na kwenda mtaa wa kapera nyumbani kwa Mandela akalala hapo kwa kisingizio hawezi kwenda katente kwa sababu pikipiki iliishiwa mafuta na ndipo walipovamiwa na mshtakiwa wa kwanza Marco Emanuel na mwenzake Elisha John wakijiita Askari Polisi kisha wakavunja mlango wakapola Pikipiki hiyo na kwenda kuiuza Kahama.
Baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na wao kukiri kuwa walifanya njama hiyo, hakimu Gabriel kurwijira amewahukumu wote wanne kwenda kutumikia kifungo jera miaka minne kila mmoja na baada ya kumaliza kifungo watawajibika kulipa kila mmoja sh.447,500 ili kulipa pikiiki , chini ya kifungu 258 na 265 kanuni ya adhabu sura namba 16 ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na matukio ya wizi wa Pikipiki kukithiri wilayani Bukombe.
Post a Comment