Header Ads

Tatizo la Maji Mjini Geita Kupungua.

Hatimaye adha ya muda mrefu ya Wakazi wa Geita kukosa maji safi na Salama huenda likamalizika baada ya mradi mkubwa wa maji uliofadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na Serikali kukamilina ambapo utazinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Samia Suluhu atakapofanya Ziara yake Mkoani Geita januari nne na tano.
Wakazi wa Geita Mjini wamekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu na kupelekea wakazi kutegemea maji ya visima na chemchem ambayo kwa usalama ni mdogo kutokana na baadhi ya vyanzo kuchafuliwa na wachimbaji wadogo na kuhatarisha afya za watumiaji.

No comments