Header Ads

HAKUNA LIKIZO JKT, KIBADENI NAYE AINGIA KATIKA MAMBO YA HAPA KAZI TU


Katika kuhakikisha JKT Ruvu haishuki daraja, kocha wa kikosi hicho, Abdallah King Kibadeni, amesema hana masihara na ameamua kuendeleza mazoezi kipindi hiki cha likizo fupi ya wiki mbili.

Hata hivyo ili kuonyesha umakini, kocha huyo amewaondoa wachezaji hao jeshini na kwenda kuwaweka nje kidogo ya jiji, Chanika.

JKT ambayo ilisimika mizizi mkiani mwa msimamo kwa muda mrefu tangu kuanza kwa ligi, kwa sasa ipo nafasi ya 10 na pointi 12, hata hivyo, King Kibadeni anasema bado hawajajihakikishia kukwepa mstari wa kushuka daraja, ndiyo maana ameamua kuendeleza program za mazoezi.

Kocha huyo mkongwe huyo amesema aliamua kuweka kambi Chanika kutokana na utulivu wa mazingira. “Kuna utulivu mkubwa huku, kama unavyojua bado tunaendelea kuimarisha timu siku hadi siku kuhakikisha haishuki daraja.


“Bado hatuko salama katika janga la kushuka daraja, ndiyo maana niliona kuna kila sababu ya kuendelea na programu za mazoezi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Simba.

No comments