Header Ads

WANANCHI GEITA WAIOMBA HALMASHAURI KUKARABATI MIUNDOMBINU.

Wananchi wa Katundu mkoani Geita wameiomba Halmashauri ya Mji huo kulishughulikia tatizo la miundo mbinu hasa barabara ambazo zimekuwa kero kubwa kwa muda mrefu si mvua wala kiangazi.
Hayo yamesemwa jana na wananchi wa mtaa wa Katundu mkoani hapa wakati PAULBAHEBE BLOG ilipopita kujionea hali ya mazingira mara baada ya mvua kunyesha na kushuhudia barabara nyingi za mitaa zikiwa katika hali mbaya.
Licha ya Geita kuwa na Rasilimali za kutosha kama madini,kilimo na utalii katika hifadhi ya Taifa Lubondo lakini imeendelea kuwa nyuma kimaendeleo hali inayoelezwa kuwa ni kutokana na ubadhilifu kwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri.
Akiongea jana wakati wa kuapishwa madiwani wa Geita pamoja na uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mbunge wa Geita vijijini Joseph Msukuma alisema kuwa kuna ubadhilifu mkubwa katika Halmashauri ya Geita akitolea mfano wa Mitambo ya kutengeneza barabara iliyoletwa ukilinganisha na kiwango cha fedha zilizotengwa ni tofauti kabisa.
Mwezi wa 3 mwaka huu Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM ulitoa kiasi cha Tshs 2.2 bilioni kama SERVICE LEVY kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Geita.
Hata hivyo kumekuwa na kashfa nyingi ndani ya Halmashauri hii zikiwemo zile za malipo hewa,ujenzi wa Stendi chini ya kiwango ambayo ilipeleka mabilioni ya shilingi.
Mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema" Tunamwomba Rais Magufuli asiishie kwenye Wizara,afike na huku kwake ili kutumbua majipu yaliyoshindikana kwani hatuoni faida ya kuwa mkoa tena anakotoka Rais wa nchi licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi"alisisitiza.

Moja kati ya barabara (balenge- jimboni) mjini Geita ikiwa na hali mbaya baada ya mvua kunyesha.
Richa ya Rais kuagiza usafi nchi nzima siku ya tarehe 9 Decemba bado maeneo mengi Geita yameendelea kuwa machafu pamoja na ma Afisa afya kuwepo mkoani hapo.

No comments