Header Ads

Barua ya Mao Zedong yauzwa $918,000.


MaoImage copyrightxinhua
Image captionMao alikuwa mmoja wa waanzilishi wa chama cha Kikomunisti cha Uchina

Barua iliyoandikwa na kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Uchina Mao Zedong akimwandikia kiongozi wa chama cha Leba cha Uingereza imeuzwa £605,000 ($918,000) kwenye mnada.
Kwenye barua hiyo ya mwaka 1937, Mao anamuomba Clement Attlee usaidizi katika kukabiliana na wanajeshi wa Japan waliokuwa wamevamia Uchina.
Wanadi wa bidhaa Sotheby wamesema barua hiyo ni ya thamani kubwa kutokana na saini ya Mao.
Bei ya mwisho ilizidi sana bei iliyotarajiwa ya £100,000-150,000.
Mnunuzi ni raia wa Uchina anayekusanya vitu vya kale.
Mao Zedong alizaliwa 1893 na ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Kikomunisti cha Uchina na mwanafalsafa msifika wa karne ya 20.

Image copyrightAFP

Alisaidia kuunga jeshi la Uchina kwa jina Red Army, na kuwaongoza kutembelea maili 6,000 kutoroka maadui wao.
Baada ya ushindi 1949, Mao alitangaza kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa Uchina na akawa kiongozi wa kwanza. Sera zake zilisababisha vifo vya mamilioni ya watu.

No comments