Header Ads

MALOPE ACHOMOZA TAMASHA LA AMANI OKTOBA 4 MWAKA HUU.

index

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Rebecca Malope, amepongeza wazo la kuwepo Tamasha la Amani linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Oktoba 4 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema tayari wasanii mbalimbali wa kimataifa wameguswa na uwepo wa tamasha hilo.
“Tumepanga kuwa na tamasha la amani Oktoba 4, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baadaye mikoa mbalimbali nchini.
“Wasanii wa Injili wa ndani na nje wamepongeza wazo hilo na wameonekana kuguswa kwa kiasi kikubwa akiwemo Malope.
“Amenijulisha kwamba tukimuhitaji yupo tayari wakati wowote kufanya naye kazi kwenye tamasha hilo. Bado tunajipanga na mambo yakiwa mazuri tutamualika,” alisema Msama.
Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

No comments