Header Ads

LAZIMA RUHUSA YA KUSHIKA MIMBA UCHINA.

Mwakamke mja mzito China
Kampuni moja imeweka sheria inayowazuia wanawake walio kwenye ndoa kushika mimba bila idhini yake
Kampuni moja ya Uchina inapanga kutoa masharti ambapo waafanyakazi wake watatakiwa kupata ruhusa kabla ya kuanza familia.
Sheria hizo zimechapishwa na kuzua malalamiko mengi katika mitandao.
Sheria kuu inaelezea kwamba wanawake wote walio kwenye ndoa lazima wawe wamehudumu kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba.
null
Anayekiuka masharti mapya na kushika mimba anatozwa faini, aidha hapati madakara
Yeyote atakayeshika mimba kinyume cha sheria hiyo atatozwa faini na kunyimwa madaraka yeyote, hata kama amefuzu.
Shirika la utangazaji nchini China limekosoa vikali kampuni hiyo iliyoko mkoa wa Henan na kusema haina ubinadamu kwa wafanyikazi wake.
Muingilio wa masuala binafsi China ni jambo rasmi, hasa sheria ya mtoto mmoja iliyowekwa na serikali miaka ya sabini. Hii iliwalazimisha wazazi wanapata mtoto mmoja pakee.BBC

No comments