Header Ads

KILA ANAYEKUTONGOZA LAZIMA UMWAMBIE MUMEO?



Wapo wanawake wenye tabia hiyo. Yuko ndani ya ndoa, uaminifu ni jambo muhimu, linajulikana. Lakini wanawake hao, kila wanapotoka kwenda gengeni au dukani kwa Mangi na kutupiwa maneno ya kutongozwa na wanaume, wakifika majumbani huwaambia waume zao.
Utamsikia mwanamke anamwambia mume wake: “Basi baba Michael leo, yule mkaka anayekaa hapo nyumba yenye kibaraza mbele nilipokuwa natoka dukani, si akanitongoza.
“Eti, anti naomba namba yako. Nikamjibu, mimi ni mke wa mtu wewe. Namba ya nini, unataka kunitafutia matatizo kwenye ndoa yangu bure. Akasema matatizo gani, kwani mumeo atajuaje?”
MBAYA ZAIDI
Ubaya wa tabia hii, mke anapoamua kusema ni kwa wanaume ambao anajua mumewe anawajua. Ndiyo maana hutaja majirani. Si rahisi mke akamtaja konda wa daladala au mwanaume aliyekutana naye kwenye daladala wakati anakwenda kumsalimia shangazi yake zaidi ya kilometa tano.
LAKINI SI WOTE
Hata hivyo, si wake za watu wote wenye tabia hiyo ya ‘kuwasemelea’ wale wanaowatongoza. Wao, uamuzi wao ni kuyaweka mambo hayo mioyoni mwao kwa siku zote za maisha.
MADHARA YAKE
Mke kusemelea ni vizuri kwani inaonesha ni namna gani anaipigania ndoa yake. Lakini pia anaonesha uaminifu katika ndoa. Lakini kwa upande mwingine, anaacha uadui kati ya mume wake na watu hao ambao yeye anapowaangalia anashikwa na hisia za wivu.
Baadhi ya wanaume hudiriki hata kuwafuata wanaume hao na ‘kulianzisha’ sekeseke la nguo kuchanika. Kisa, mkewe kamwambia jamaa huyo anamsalandia.
JE, KILA ANAYEKUTONGOZA LAZIMA UMWAMBIE MUMEO?
Naamini hapa ndipo penye hoja ya msingi na panapotaka maarifa zaidi badala ya kuangalia kwa juujuu.
WANAUME WANAPISHANA
Ukiuliza wanaume wengi kuhusu tabia hii ya wake zao kuwataja kwa wanaume zao wale wanaowatongoza, watatoa majibu tofauti kutokana na kila mmoja na mtazamo wake.
Wapo wanaume hawataki kusikia, wapo wanaume wanaotaka na kuona ni sawasawa tena huwafagilia wake zao kwamba, ni waaminifu sana ndiyo maana wanakuwa wanasema kwa kila mwanaume anayemtongoza.
Lakini hata hivyo, wanaume wenye kuchekecha akili sawasawa kabla ya kutoa majibu wanatilia shaka kitendo hicho wakiamini kwamba, wanawake wenye tabia hiyo ni wale ambao kama itatokea akamkubali mwanaume huyo anayemtongoza, maana yake ni nini?

No comments