JERRY MURO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, MSIBA UKO UBUNGO MAZIWA.
JERRY MURO |
Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amefiwa na baba yake mzazi.
Babaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa kwa siku kadhaa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Muro amesema msiba uko nyumbani kwa marehemu Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.
"Kama unavyojua kwa sisi Wakristo, kidogo taratibu zinakwenda kwa kusubiliana. Hivyo msiba ni pale Ubungo Maziwa nyumbani kwa marehemu," alisema Muro.
MUNGU AMPUMZISHE MZEE MURO KWA AMANI.
Post a Comment