Vitambulisho 134 vya mpiga kura vyakamatwa na TAKUKURU mkoani Kagera.
Vitambulisho 134 vya Kupigia kura, vimekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU- mkoani Kagera baada ya kukutwa vimenunuliwa na Kundi la watu kutoka kwa wapiga kura.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Naibu mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John Joseph vitambulisho hivyo vimekamatwa vikiwa tayari vimenunuliwa kutoka kwa wananchi kwa bei ya kati ya shilingi 5,000 hadi 10,000.
Amesema kuwa kukamatwa kwa Vitambulisho hivyo, kumetokana na baadhi ya Vijana walioshawishiwa kuuza kadi hizo na kundi la watu wanaopita, kutoafiki na kisha kulazimishwa kufanya hivyo.
Post a Comment