MASIKINI MAMA HUYU KWA MAUMIVU ANAYOYAPATA AOMBA KUKATWA MGUU.
JAMII imeombwa kutoa msaada wa hali na mali kwa BI GRACE KAIZA mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye ameomba mukatwa mguu wake kutokana na Saratani ( Kansa) katika mguu huo.
Bi. Grace Kaiza amesema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu jambo lililomuathiri kwa kiasi kikubwa kiafya na hata kiuchumi.
Akielezea namna tatizo hilo lilivyompata amesema lilianza kama uvimbe katika mguu wake kisha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini haikusaidia na ndipo alipobainika kuwa na ugonjwa huo
Ameongeza kutokana na ugonjwa huo amekuwa akipata maumivu makali mno yanayo mliza hasa nyakati za usiku hali inayomfanya kushindwa kulala.
Msamalia mwema ambaye pia nimjumbe wa serikali ya mtaa wa NYAKATO MAHANGO Jijini Mwanza BI KHADIJA YASIN amesema kuna haja ya kumsaidia BI GRACE kutokana na shida anazopata.H abari na Mjengwa blog.
Post a Comment