MAMIA YAMUAGA MWANDISHI KAMUKARA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.
MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa Juni 29 mkoani Kagera. Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson Kamukara wamesema ni pigo kwa tasnia ya habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .
Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha. “ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbowe Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha. “Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema Mengi.Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. Safari ya kuelekea Kagera kwaajili ya maziko ya Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.(MICHUZI)

Post a Comment