Header Ads

Daraja la Kwatamara Kata ya Bulega wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Lavunjika.


Muonekano wa Daraja la KWATAMARA lililokatika kutokana baada ya maji mengi kushidwa kupita katika matundu ya daraja hilo na kupita juu. Daraja hilo lipo katika Kata ya Bulega wilaya ya Bukombe Mkoani Geita. 

Picha/Habari Gibson Mika -Radio Geita.

Wakazi  wa kata ya Bulega wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita wameiomba Serikali kuwajengea daraja la KWATAMARA ililokatika hivi karibuni na kusababisha bei za vinywaji na usafiri na kupanda hali inayowapa shida hasa wa kipato cha chini.


Wakizungumza na Radio Kwizera baadhi yao Mashashi Mwenda, Pendo Makoye na Leonard Malimi  wamesema kutokana na mvua iliyonyesha hivi karibuni katika kata hiyo ilisababisha daraja hilo kukatika na kukata mawasiliano baada ya daraja hilo kusombwa na maji  hali ambayo imesababisha bei ya soda 1 kupanda kufikia sh.700 huku bei ya usafiri ikifikia shilingi elfu 6 badala ya shilingi elfu 3 kufika makao makuu ya wilaya hiyo.

Hata hivyo wameiomba Serikali kuwatengenezea barabara hiyo ili kurahisisha shughuli za usafirishaji wa bidhaa kuzifikisha katika soko la BULEGA lililopo katika kata hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe MHE. DOTTO MASHAKA BITEKO amewataka Wananchi kuwa wavumilivu na kwamba amefanya  mazungumzo na kampuni ya ujenzi wa barabara STRABAGiliyopo wilayani humo kwa lengo la kuwasaidia wananchi kuwatengenezea barabara hiyo na kwamba tayari wamekwisha kufika eneo hilo kwa ajiri ya utafiti wa awali kabla ya kuanza ujenzi.

No comments