Nape Akoleza Moto Hoja ya Bashe
Mbunge wa Mtama (CCM) Ndugu Nape Nnauye amewataka Wabunge wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kumuunga mkono Mbunge Hussein Bashe juu ya hoja yake binafsi aliyoiwasilisha kwa Katibu wa Bunge.
Nape ametoa kauli hiyo jana (Machi 07, 2018) baada ya kupita siku kadhaa tokea Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe kudai amepeleka barua kwa Katibu wa Bunge na kupelekea kuibuka kwa baadhi ya wabunge wa upinzani kumpinga na kumuita mnafki kwa anachokitarajia kukifanya.
"Kazi ya Mbunge ni pamoja na kuwasemea wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hawana fursa ya kwenda wenyewe Bungeni. Tumuunge mkono Mhe. Bashe bila kujali tofauti zetu za itikadi, dini au rangi", amesema Nape.
Kwa upande mwingine, Nape amedai hoja binafsi ndani ya Bunge ni moja ya njia za kutafuta ukweli na suluhisho juu ya jambo fulani ambalo linatafutiwa ufumbuzi wake.
Post a Comment