KCMC yatoa taarifa ya maendeleo ya afya ya Mhe. Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa, ameeleza Afisa Habari wa KCMC.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu hii, Ofisa habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema walimpokea Mbowe jana jioni Machi 4, 2018 akiwa na maumivu makali ya kichwa.
Amesema hali ya Mbowe inaendelea vizuri na amepumzishwa hospitalini hapo.
“Jana jioni tulimpokea Mbowe, taarifa zinaonyesha alikuwa na maumivu ya kichwa. Taarifa za kitabibu zinaonyesha ni uchovu,” amesema Chisseo.
Amesema madaktari wanaendelea kumhudumia kwa ukaribu na baadaye atafanyiwa vipimo vingine.
Post a Comment