Harry Kane atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
Mchezaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa London Football (London Football Awards).
Harry Kane akiwa na tuzo ya London Football Awards
Katika kinyang’anyiro hicho cha mchezaji bora wa mwaka, Kane ameshindana na Cesar Azpilicueta, Heung-Min Son, Christian Eriksen na Wilfried Zaha.
Kocha wa Crystal Palace, Roy Hodgson akizawadiwa tuzo meneja bora wa mwaka
Meneja wa Crystal Palace, Roy Hodgson ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka katika sherehe hizo zilizofanyika Battersea Evolution.
Ryan Sessegnon (kushoto) akiwa na Sol Campbell akiwa na tuzo yake
Katika sherehe hizo aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza amepewa tuzo ya heshima huku Ryan Sessegnon akitwaa ya uchezaji bora wa mwaka wa EFL.
Meneja wa West Ham, David Moyes akiwa amewasili Battersea Evolution
Post a Comment