Meza kuu ikiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali na chama cha mapinduzi.
Na,Consolata Evarist,Geita
Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita,Wilayani Halmashauri ya Mji Geita limepitisha makadirio ya bajeti ya matumizi ya ya mwaka wa fedha 2018/2019 kiasi cha shilingi Bilioni 44,983,764,197.00 katika shughuli mbalimbali za Halmashauri. Kati ya Fedha hizo Jumla ya Tsh 15,585,248,344.00 ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ikiwa ni Mapato ya Ndani, Ruzuku ya Serikali na Wahisani mbalimbali. Tshs. 4,765,976,688.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikali kuu na Mapato ya ndani na Tshs. 24,632, 539,165.00 kwa ajili ya mishahara.
Aidha Halmashauri imekisia kukusanya Jumla ya Tsh 5,114,157,735.00 toka vyanzo vya ndani ambayo fedha hii imejumuishwa katika jumla ya Bajeti ya mwaka 2018/2019. Jumla ya Tsh. 3,030,016,641.00 sawa na 60% zimetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Akiongeza katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita kwenye kikoa cha kupitisha bajeti ya Mwaka wa fedha 2018/2019,Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali alisema Bajeti hyo imezingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa kuandaa Bajeti uliotolewa na Wizara ya Fedha Mwezi, Novemba 2016, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030); Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, Mpango wa Pili wa miaka Mitano (FDYPII) 2016/17-2020/21 na Lengo likiwa ni kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2030.
“Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019,kwenye halmashauri hiyo kuwa imejielekeza katika kufikia vipaumbele vyenye shabaha na malengo yafuatayo Kuendelea kuboresha na kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani ili kuongeza mapato ya Halmashauri. Kuboresha Sekta za huduma za jamii, hususan, Elimu, Afya, Maji,Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Misitu, Maendeleo ya Jamii, Ushirika.Kusaidi Sera ya Taifa kufikia Uchumi wa kati wa uendelezaji wa viwanda.Kuimarisha Utawala bora”Alisema Modest
Aidha ameongeza kuwa Halmashauri inategemea kukusanya mapato yake kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama kodi ya huduma( service levy) kutoka kampuni ya Mgodi wa Dhahabu Geita na Kampuni nyingine zinazofanya kazi na Mgodi huo, kodi ya nyumba za kulala wageni, Leseni za biashara,faini mbalimbali, upigaji chapa mifugo na ushuru wa mifugo, ushuru wa mazao mbalimbali na matunda.
“Katika Bajeti ya mwaka 2018/2019. Jumla ya Shilingi 15,585,248,344 zimetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, Kiasi cha shilingi 24,632,539,165 kwa ajili ya mishahara ya watumishi na Shilingi 4,765,976,688 kwa ajili ya matumizi mengineyo”. Aliongeza Mhandisi Aporinaly
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita Mheshimiwa Leonard Kiganga Bugomola alisema kwa mwaka wa fedha uliopita Halmashauri ilipanga kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 5, ambapo hadi kufikia mwezi Disemba 2017 Halmashauri imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi 2,868,353,850.15 sawa na asilimia 52.
Mh. Bugomola ameongeza kuwa kutokana na mafanikio ya ukusanyaji uliofikia nusu ya makadirio ana imani kuwa mpaka kukamilisha mwaka wa fedha 2017/2018 mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri itakuwa imefikisha lengo la makusanyo. Aidha makusanyo hayo yanatoa mwanga wa mafanikio katika bajeti iliyopitishwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amewasisitiza wajumbe kuwa na ukusanyaji mzuri wa mapato hili kuweza kutekeleza bajeti kwa uzuri zaidi.
Katika Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Halmashauri ya Mji Geita imejielekeza katika kufikia vipaumbele vyenye shabaha na malengo ambayo ni Kuendelea kuboresha na kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani ili kuongeza mapato ya Halmashauri, Kuboresha Sekta za huduma za jamii, hususan, Elimu, Afya, Maji, Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Misitu, Maendeleo ya Jamii, Ushirika,
Kusaidia Sera ya Taifa kufikia Uchumi wa kati wa uendelezaji wa viwanda na Kuimarisha Utawala bora.
|
Post a Comment