Freeman Mbowe aruhusiwa kutoka hospitali. Daktari aeleza ugonjwa wake
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) ameruhusiwa kutoka hospitali hapo baada ya madaktari kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika.
Mbowe alilazwa hospitalini hapo kuanzia juzi usiku ambapo alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.
Afisa Habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema kuwa Mbowe ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo, baada ya madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kuona afya yake inazidi kuimarika.
Mbowe alifikishwa KCMC Machi 4 akiumwa kichwa, na jana Machi tano aliruhusiwa kutoka hospitalini.
Post a Comment