WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO MJINI GEITA
Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondary ya Mwatulole,Bi Roselyine Mdariki akishukuru kuwenza kupatiwa msaada huo kwenye shule hiyo ambao utasaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. |
Mzee Devid Ng’ombeyapi akielezea namna ambavyo aliguswa na kuamua kuchangia kwenye sekta ya Elimu. |
Baadhi ya vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondary Mwatulole. |
Mzee Devid Ng’ombeyapi akibidhi theruji kwa Diwani wa kata ya Buhala hala( kushoto) Musa Kabese Pamoja na kwa mkuu wa shule ya Sekondary ya Mwatulole Bi,Roselyine Mdariki. |
Wananchi katika Halmashauri ya mji wa Geita wametakiwa kuendelea kuunga Mkono jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya Elimu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mhandisi Modest Apolinary wakati akipokea mifuko 10 ya theruji na tripu mbili za mchanga kwenye shule ya sekondari ya Mwatulole kutoka kwa mwananchi aliyejitolea kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni shuleni hapo.
Alisema suala la kutoa michango halijakatazwa,kilichozuiwa ni walimu kujihusisha na kupokea michango ama kuwarudisha wanafunzi kwa sababu ya kutotoa michango jambo ambalo sio sahihi na kwamba kwa mtu ambaye anaguswa ni vyema wakawasiliana na ofisi ya mkurugenzi mtendaji.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Mwatulole Bi,Roselyine Mdariki mbali na kushukuru kwa msaada huo ameelezea changamoto ambayo wanaipata kwa sasa shuleni hapo ni upungufu wa madarasa kwani kwa mwaka huu wamepokea wanafunzi wengi zaidi wa kidato cha kwanza ukilinganisha na miaka iliyopita.
“Shule yetu imekuwa na changamoto ya vyumba vya madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi kwa mwaka huu na kutokana na ongezeko hilo mkurugenzi wetu wa halmashauri ameamua kutuunga mkono kwa kutupatia mifuko ya seruji mia moja tunaamini itasaidia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapa”Alisema Mdariki.
Hata hivyo diwani wa kata ya Buhalahala,Musa Kabese ,alisema changamoto kwenye kata yake ni upungufu mkubwa wa madarasa ambapo vinahitajika vyumba kumi na moja ili kukidhi mahitaji kwa shule mbili za sekondari mwatulole pamoja na kalangalala .
Kwa upande wake mwananchi ambaye ametoa msaada huo,Devid Ng’ombeyapi alisema wanafunzi kuhangaika kutokana na uhaba wa madarasa ndicho kilichomsukuma kutoa msaada huo.
Post a Comment