MTOTO WA MIAKA SITA AFARIKI WAKATI AKIOMBEWA MAPEPO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kufariki kwa mtoto wakati alipokuwa akiombewa.
Na,Joel Maduka,GEITA
|
Mtoto wa miaka sita (6) ambaye anajulikana kwa jina la Frank Bariki amefariki wakati alipokuwa akiombewa mlimani alikopelekwa kwa ajili ya kutolewa mapepo kwa madai kuwa alikuwa na taswira ya Bibi yake,huku mama mzazi akishikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo alisema Tukio hilo lilitokea february 18,2018 majira ya saa tano asubuhi katika mlima wa Gambiwe kwenye kijiji cha Bukuru Wilaya ya Nyang’hwale.
Aidha amewataja wanawake hao kuwa ni Bi,Neema Petro(25) ambaye ni mama wa mtoto huyo na mke mwenzake Raheli Mussa (25) ambao wameolewa na Bw,Bariki Lunyaru walikuwa kwenye kipindi cha mfungo wakiwa kwenye maombi yao wakati wakimuombea kwa ajili ya kumtoa mapepo ndipo walianza kumkamia mtoto huyo wakimshika na kumkaba kwenye mbavu na kwenye shingo hali ambayo ilipelekea mtoto huyo kupoteza maisha.
Kamanda Mponjoli ameendelea kusema wamechunguza mwili wa mtoto wamebaini kulikuwa na alama za mikwaruzo kwenye maeneo ya shingoni na kwenye mashavu .
Ameendelea kufafanua kuwa hadi sasa bado hawajajua kiini cha tukio hilo ambalo limesababisha mtoto huyo kupoteza uhai wakati alipokuwa akifanyiwa maombi ingawa hadi sasa jambo ambalo wamebaini kuna viashiria vya vitendo vya ushirikina ndani ya familia kutokana na madai ya taswira ya bibi yake .
Kamanda Mponjoli alisema hadi sasa wanawashikilia wanawake hao ambao ni wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang’hwale kutokana na kifo cha mtoto huyo.
Post a Comment