Bwawa la Maji la Kunyweshea mifugo likiwa kwenye eneo ambalo ni karibu na sehemu ya Kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu.
Wananchi wa Kijiji cha Ililika Kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita wameandamana kupinga mwekezaji kuweka kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu kwa madai kuwa chanzo cha maji ambacho wanakitegemea kijijini hapo kipo karibu na planti ambayo inajengwa na kwamba inaweza kusababisha madhara ya afya kutokana na Kemikali yaCyanide ambayo hutumika kwenye shughuli za uchenjuaji.
Wakizungumza na mtandao wa BAHEBE STAR kwa vipindi Tofauti wamesema kuwa hofu kubwa waliyonayo ni kutokana na sumu ya kuchenjulia dhahabu kwani ni hatari kwa afya zao na viumbe ambavyo vinazunguka maeneo ambayo wanafanyia kazi.
“Sehemu hii ni karibu sana na eneo ambalo tunachotea maji sasa kama wakiweka hicho kiwanda sisi wananchi tutakuwa kwenye hali gani hebu serikali ijaribu kulitazama swala hili kwa umakini zaidi tutaisha kutokana na sumu ya kuozesha marudio”Alisema Bi,Hellen Mbaru.
“Sawa eneo hili ni la mtu Binafsi na lipo ndani ya kijiji cha Ililika na kwamba tunaambiwa kuwa watawapa angalizo wawekezaji ndani ya mwaka mmoja endapo kama kuna maafa ambayo yatajitokeza watawafukuza kweli na hali hii jamani hadi watu wadhurike ndio tahadhari ichukuliwe mimi naomba sana serikali ilitazame hili”Alisema
Hata hivyo Lawama nyingi zimemwangukia Mwenyekiti wa Kijiji kuwa amehusika kwa kiasi kikubwa Kwa kuchukua rushwa kutoka kwa mwekezaji na kwamba kwa sasa hawana imani naye hali ambayo imesababisha kufunga ofisi ya Kijiji.
Kutokana na hali hii askari Polisi wamefika kwenye eneo hilo na kumshauri Mwenyekiti wa Kijiji hicho ambaye alifika kwenye eneo hilo kuona umuhimu wa kuwasikiliza wananchi na kusitisha ujenzi wa Planti hiyo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Daniel Mwigulu Nkela,amesema kuwa maamuzi ambayo yalichukuliwa hayakuwa ya peke yake bali ni ya wajumbe wote ambao waliridhia eneo hilo kujengwa planti.
“Maana ya serikali kuna wajumbe 25 mimi kama mwenyekiti sina mamlaka ya kuidhinisha eneo hili peke yangu mwekezaji anapotaka kuingia tunaitisha serikali ya kijiji inakaa na inapokaa kuna kuwa na mahojiano kati ya mwekezaji na wajumbe wa serikali ya kijiji mimi kazi yangu ni kulinda maadhimio kikao tu sina mamlaka ya kuidhinisha eneo lolote lile”Alisema Mwigulu.
Bahebe star imemtafuta mwekezaji wa eneo hilo kutaka kujua makubaliano yake na serikali ya kijiji ambapo moja kati ya wasimamizi wa eneo wamegoma kuzungumzia swala hilo na kwamba anaye weza kuzungumzia swala hilo ni meneja wao ambaye yupo Mwanza kwa sasa hata hivyo jitihada bado zinaendelea kujua makubaliano yalikuwaje.
|
Post a Comment