Katibu Mwenezi wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Jonathan Masele akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama cha mapinduzi leo.
Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Geita kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Jitihada ambazo ameendelea kuzifanya ikiwa ni pamoja na kufichua uovu kwa baadhi ya sekta za serikalini pamoja na watumishi ambao wameendelea kuhujumu uchumi wa nchi bila ya kuwa na sifa za kazi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake ,Katibu wa siasa na uenezi wa Chama hicho Wilaya ni Geita Jonathani Masele ,amesema kuwa shughuli na jitihada ambazo zimeendelea kufanywa na Rais Magufuli sio za kubezwa na Watanzania kwani ni muda mrefu watu wamekuwa wakijifanyia mambo na kujinufaisha Bila ya kuangalia manufaa ya Nchi.
“Tunatambua kazi ambazo anazifanya Mheshimiwa Rais sio za kubezwa kabisa kama ambavyo tumeona miaka mingi Migodi ilikuwa ikisafirisha mchanga bila hata ya watanzania kujua lakini yeye amefichua yote ambayo yalikuwa yanaendelea Mimi namuomba Rais aangalie kwa wachimbaji wadogo kwani baadhi yao wamekuwa na tabia ya kujibinafsishia maeneo mwisho wa siku wanabadilisha majina bila hata ya kuyatumia maeneo hayo na ni vyema wakanyang'anywa ili wapatiwe wale ambao wana uwezo wa kuendelea kuyatumia”Amesema Masele.
Mwenyekiti wa Wilaya Hiyo ,Barnabas Mapande akizungumza kwenye Kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya chama hicho amemtaka Rais kutokuwasikiliza wale ambao wamekuwa wakimlalamikia kwa hatua anazozichukua.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye ni mmoja kati ya wajumbe wa kikao hicho amewasisitiza wajumbe na wanachama kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye maswala ya elimu pamoja na afya huku akisisitiza kuwa yeye kama mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani humo atahakikisha kuwa Mgodi ambao upo kwenye Wilaya ambayo anaiongoza kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wanasimamia kwa umakini dhahabu ambazo zinasafirishwa kwenda nje ya nchi.
Kamati ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM imekutana leo lengo likiwa ni kujiandaa na uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya chama hicho.
|
Post a Comment