Teknolojia: Mkanda wa Kiunoni Unaojikaza na Kujilegeza Wenyewe.
Kuna simu janja, saa janja n.k, na mwaka huu kampuni moja kutoka nchini Ufaransa umetambulisha mkanda janja – kimombo ‘smart belt’.
Mkanda huo uliopachikwa jina la Belty unateknolojia unayoiwezesha kujilegeza na kujikaza kulingana na ukaaji wako au kushiba kwako.
Mkanda huo utakaoweza kuwasiliana na simu yako kupitia app yake, utaweza kukupa data muhimu kuhusu kipimo cha kiuono na data zingine kama vile kama unanenepa au unapungua n.k.
Kama mara nyingi ilikuwa inakubidi kulegeza mkanda baada ya mlo basi utasahau shughuli hiyo tena, mkanda huu utaweza kujiweka vizuri wenyewe, kimombo kuji’adjust’ kulingana na hali yako. Kwa kifupi utakuwa unaweza kujua kama kuna hali ya kukubana inatokea na hivyo itajilegeza kidogo na ikiona kuna kupwaya basi utajivuta kidogo.
Kama unaupendeleo wa kipimo flani basi utaweza kuchagua mwisho wa mkanda huo kujifunga – yaani kama unapendelea mkanda unaoachia nafasi kubwa zaidi bila kukubana.
Kampuni inayotengeneza mikanda hiyo bado haijasema ni lini rasmi mikanda hiyo itaanza kupatikana ila kwa sasa inaonekana kwa kiasi kikubwa itaingia sokoni mwakani. Haitauzwa bei rahisi na hivyo kuweza kuupata mkanda huo lazima ujitayarishe kutoa madolali kadhaa.
Post a Comment