Header Ads

MTOTO AUWAWA KIKATILI GEITA.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi juu ya tukio la mtoto aliyeuwawa.


Bi,Elizabeth Selemani ambaye ni mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili akielezea mazingira ya mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho. 



Mtoto wa umri wa mwaka mmoja na miezi saba ambaye  jina lake tumelihifadhi  ameuwawa kikatili na kuchomwa na moto  sehemu za makalio.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nyalubanga ,kata ya Lwezera Wilaya na Mkoa wa Geita , ambapo anayesadikika kufanya tukio  hilo ni Baba wa Kambo anayejulikana kwa jina la Petro Bahati(35).msukuma mkazi wa kijiji hicho.

Akizungumzia tukio hilo Mama mzazi wa mtoto aliyefariki Bi,Elizabeth Selemani ameelezea kuwa wakati tukio hilo linatokea yeye alikuwa Bafuni akioga na mtoto alimuacha mume wake akiwa na mtoto ambaye ni marehemu kwa sasa .

Bi,Elizabeth ameendelea kueleza kuwa alipokuwa akikoga alikuja mume wake akiwa na hasira na kumwomba kanda mbili kuwa hampatie ili haondoke mala baada ya kupatiwa aliondoka huku akimwacha bafuni na kuelekea kusiko julakana na baadae aliporudi ndani alimkuta mtoto akiwa amekalishwa alipomsogelea alimkuta akiwa na majeraha sehemu za shingoni na kwenye makalio akiwa amechomwa moto hali ambayo ilimpelekea kutoa taarifa kwa majirani.

“Nilikuwa ninaishi nae vizuri tu wala hakuwa na tatizo kwa mtoto sijui ni nini ambacho kimempata hadi kufikia hatua hii yani hata na mimi nimechanganyikiwa kwakweli”Alisema Elizabeth.

Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita ,Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa wa tukio hilo hajakamatwa na wanaendelea na juhudi za kumtafuta ili aweze kufikishwa kwenye Mkono wa sheria. Na kwamba tukio hilo ni la pili kwa maeneo hayo.

Huku akitoa rai kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya kikatili kama vya namna hiyo kuacha mara moja kwani jeshi hilo alitasita kuchukua hatua kari za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.



Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Geita,ambaye pia ni mkuu wa wilaya Mwl Herman Kapufi amechukua nafasi hiyo kuwahasa wanananchi  hususani ni wasichana na wanawake kuwa waangalifu pindi wanapotaka kuolewa na watu wasio wajua.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

No comments