Mahakama Nchini Kenya Yatoa Amri ya Kuwakataa Madaktari wa Tanzania
Mahakama ya Kazi nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.
Jaji Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo ametoa amri hiyo baada ya Madaktari watano wa Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango wake wa kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari wengi nchini humo ambao hawajaajiriwa.
Madaktari hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari 1,400 ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na iizuie serikali kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa afya kutoka nje.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli kukubali ombi lilitolewa na Rais Uhuru wa kuipatia Kenya madaktari katika kusaidia utoaji tiba baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo wenye lengo la kushindikiza waboreshwe maslahi yao.
Post a Comment