Header Ads

'Yesu nipe nyonyo‘: Wimbo Ambao Kenya Inataka Uondolewe Mtandaoni Kwa Kudhalilisha Dini

Gazeti la Kenya liitwalo taifa leo limeripoti kwamba bodi ya filamu kwenye nchi hiyo imehuzunishwa na Msanii wa muziki wa Injili SBJ kuimba wimbo wa Injili ambao unadhalilisha Imani.

Wimbo wenyewe unaitwa ‘Yesu nipe nyonyo‘ ambapo mkuu wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alisema baadhi ya Waimbaji wa Kenya wamekosa maadili na kipaji cha kubuni au kutunga nyimbo nzuri zisizochafua hali ya hewa.

Alisema wimbo huo unaendelea kukaguliwa kwa sababu Wakenya wamekasirishwa: "Nashangaa sana mtu mzima anakaa chini na kuimba wimbo kama huu, Wasanii wetu wamejua kuwa kama hawaongei uchafu ama kutoa video za utata hawatasikilizwa wala kutazamwa na wanafanya hivyo ili wapate umaarufu”

Tayari bodi hiyo ilikua kwenye mipango ya kuwaandikia Youtube ambao ndio wanamiliki wa mtandao huo ili waiondoe hiyo video kwasababu bodi hiyo inayo mamlaka na katiba haitakubali Wasanii kutunga nyimbo za kudhalilisha imani.

Mpaka sasa wimbo huo bado upo kwenye mtandao na umeshatazamwa mara 93,812 mpaka sasa.
 

No comments