Header Ads

Watano wahofiwa kufa maji Ziwa Victoria.

Ziwa Victoria 

Muleba: Watu watano wanahofiwa kufa maji baada ya boti walilokuwa wakisafiria kupinduka jirani na Kisiwa cha Mazinga kwenye Ziwa Victoria.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango alisema boti hilo lilizama jana.

Alisema uongozi wa wilaya umetoa mafuta kwa ajili ya boti ili kwenda kutafuta  miili ya watu hao. Aliwaomba wananchi na hasa wavuvi kutoa ushirikiano kuhakikisha inapatikana.

Source: Mwananchi

No comments