Mkurugenzi wa JamiiForums kutetewa na jopo la mawakili sita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo .
Dar es Salaam. Wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo akiendelea kusota rumande, jopo la mawakili sita akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu wamejitokeza kumtetea iwapo atapelekwa mahakamani.
Mawakili wengine walioonyesha nia ya kumtetea Melo ni Peter Kibatala, Ben Ishabakhaki, Jeremiah Mtobesya, Jebra Kambole na Nazakiel Tenga.
Jopo hilo jana liliwasilisha maombi Mahakama Kuu ya Tanzania kuhoji uhalali wa Jeshi la Polisi kuendelea kumshikilia Melo bila kumfikisha mahakamani.
Jana saa 11 jioni, gazeti hili liliwasiliana na mmoja wa mawakili hao, Jebra Kambole ambaye alisema hadi muda huo polisi walikuwa bado wamemshikilia Melo na kwamba, hawatatoa dhamana hadi hapo jalada lake lililopo kwa Mwanasheria wa Serikali litakaporejeshwa na kufikishwa mahakamani.
Post a Comment