Wakazi wa Mtaa wa Magema na Nyamalembo waulalamikia Mgodi wa GGM
HABARI:GEITA INFO
Wakazi wa Mtaa wa Nyamalembo na Magema wamelalamika juu yakuzuiwa kufanya shughuli za kimaendeleo katika maeneo yao na Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kuwa wako ndani ya Leseni ya Mgodi na hivyo kukosa huduma za kijamii kama maji,shule,masoko na vituo vya afya.
Wakazi hao wameiomba Serikali sasa kuingilia kati kwani wanashindwa kufanya shughuli za kimaendeleo hali inayowapa wakati mgumu kwani hawawezi kufanya shuguli za kuwaingizia kipato kama uchimbaji,ulimaji na hata ufugaji wa mifugo.
Post a Comment