Header Ads

JIFUNZE MAMBO MUHIMU KUTOKA KWA WATU WENYE MAFANIKIO.



Ipo haja kubwa sana ya kujifunza kupitia watu waliofanikiwa ili kuweza kufikia mafanikio mkubwa. Kupitia maisha yao kuna mambo mengi ya msingi tunakuwa tunajifunza na kuachana na makosa ambayo wao waliyafanya bila kujua.

Na kiuhalisia yapo mambo mengi ya kujifunza kutoka watu waliofanikiwa ambayo yanaweza kuwa msingi mkubwa wa mafanikio yetu. Kuyajua mambo hayo itakusaidia kujiamini na kuendelea mbele. Mamba hayo ya kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa ni kama haya yafuatayo:-

1. Watu waliofaniwa ni watu wa kutegemea mafanikio makubwa kutoka ndani mwao na siyo kinyume cha hapo. Ni watu wa kuamini ule uwezo walionao ndani mwao kuwa ndiyo utakao wafanikisha.

2. Watu waliofanikiwa ni watu wa kuishi kwa bajeti. Mara nyingi hujikuta wakikata au kupunguza kile ambacho siyo cha muhimu katika bajeti yao na kutengeneza bajeti upya itakayowafanikisha. Kwa kifupi, matumizi yao kwa sehemu kubwa yanaongozwa na bajeti.

3. Watu waliofanikiwa ni watu wa vitendo. Mara nyingi siyo waongeaji sana. Ni watu wa kuchukua hatua ambazo zinaleta matokeo halisi na chanya yatakayojitokeza kwenye maisha yao.

4. Watu waliofanikiwa wako makini na suala zima la uwekezaji. Kila wakati wamefungua macho yao kuangalia ni wapi ambapo wanaweza kufanya uwekezaji ambao utawaletea matunda na mafanikio makubwa badala ya kukaa na kutumia pesa hizo tu.

5. Watu wenye mafanikio wanatumia muda wao mwingi kujifunza. Kwa kifupi hawa ni watu wa kujifunza kupitia kusoma vitabu mbalimbali hata pia kuhudhuria semina au warsha za mafanikio.

6. Watu wenye mafanikio ni watu kuendelea mbele hata pale inapotokea wameshindwa katika jambo fulani. Huwa hawasimami kusikilizia sana maumivu hayo. Hujifunza na kisha safari ya mafanikio kuendelea kama kawaida.

7. Watu wenye mafanikio mara nyingi wanazungukwa na watu wenye mitazamo chanya kama ya kwao. Watu hawa wanaowazunguka huwasaidia zaidi kimtazamo na kuwafanya wawe na mafanikio muda wote.

8. Watu wenye mafanikio hawana kauli za kushindwa kwenye maisha yao. Muda mwingi wamebeba kauli za mafanikio. Hutaweza kuja kuwasikia wakisema ‘siwezi hili, au lile’ badala yake hukaa na kusema ‘nitaweza vipi kufanya jambao hili nakufanikiwa’ hizo ndizo kauli za watu wenye mafanikio.

9. Watu wenye mafanikio ni watu wa kujitoa mhanga. Siku zote wako tayari kufanya na kutoa chochote ili mradi tu mipango na malengo ya iweze kutumia na kufika kule wanakotaka kufika.

10. Watu wenye mafanikio ni watu wa kufanya mambo yako kwa kuweka nguvu nyingi za uzingativu katika eneo moja. Kama kuna jambo wameamua kulifanya wanaling’ang’ania hilohilo mpaka liwape matokeo kamili.

11. Watu wenye mafanikio ni watu wa kutunza muda siku zote. Hawako tayari kupoteza muda wao kwa kufatilia mambo ambayo wanaona hayana msaada kwao.

12. Watu wenye mafanikio ni watu wenye uvumilivu wa kutosha. Kuna wakati huwa wanashindwa katika mambo yao, lakini huvumilia mpaka kuweza kufanikiwa.

Yapo mambo mengi sana ambayo unaweza kujifunzakupitia watu waliofanikiwa, lakini unaweza ukayafanyia kazi mambo  hayo kwanza ili yawe msingi bora katika safari yako ya mafanikio uliyonayo.

No comments