Header Ads

VIDEO: Miss Honduras na Miss Mexico wakiimba Hainaga Ushemeji ya Manfongo.

Mrembo anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World 2016 Diana Edward usiku wa December 8 2016 akiwa katika kambi ya Miss World 2016 Marekani, alipost video fupi katika account yake ya instagram akiwa na ma-miss wenzake wakiimba wimbo wa Manfongo.

Diana alipost video hiyo akiwa pamoja na Miss Honduras 2016 Kerelyne Campigotti na Miss Mexico 2016 Anna Girault wakiimba wimbo wa kisingeli wa Hainaga Ushemeji wa Manfongo wakiwa katika kambi ya Miss World.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Miss Tanzania 2016 Diana Edward yupo Marekani kwa ajili ya mashindano ya Miss World 2016, fainali ya mashindano hayo itafanyika December 18 2016.

No comments