Header Ads

Sababu za Darasa na Mavoco kumtaja Samatta kwenye nyimbo zao.

Ngoma nyingi zimeachiwa hivi karibuni za wakali wa Bongo flavor, kati ya ngoma hizo ni pamoja na heat song iliyofanywa na Darasa kwa kumshirikisha Ben Paul ngoma inajulikana kama MUZIKI, lakini pia Richi Mavoco akishirikiana na Diamond Platnumz wametoa wimbo wao unaitwa KOKORO.

Nyimbo zote hizo mbili ukizisikiliza utasikia kuna sehemu anatajwa mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anaekipiga kwenye klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

Kuna sababu kubwa ya kujiuliza kwa nini Samatta anatajwa kwenye ngoma hizi zinazobamba kwa sasa kwenye vituo mbalimbali vya radio na TV za Bongo na nje ya mipaka ya Bongo, na hii ndio sababu ya kumtafuta Darasa na Mavoco wakuambie kwanini Samatta ametajwa kwenye ngoma zao.

“Samata nimemtaja kwa maana moja, kuwa-inspire vijana kama kina Samatta mtaani kwa ajili ya kupambana bila kujali position ambazo wanazo, kuwatengenezea mazingira ya wao kujituma zaidi na kutengeneza mazingira kwa ajili ya watu wanaojituma waone thamani ile waliyonayo kina Samatta na kuingia kwenye mkumbo wa kujituma ili tuwe na kina Samatta wengi.”

“Ukiangalia kwenye mataifa yaliyoendelea watu kama kina Cristiano Ronaldo watu wanawapa heshima wanawaonesha kiasi gani nchi haing’ai bila ya wao.”

“Sijawahi kuongea na Mbwana Samatta wala sijui kama ni shabiki wa nyimbo zangu wala sitaki kujua, nilichotaka kufanya ni kumpa thamani ambayo anastahili kupewa.”

Kwa upande wa Rich Mavoco yeye anasema kwamba, kwa ukali wake alionao kwenye muziki hapa Tanzania au Afrika Mashariki kwa ujumla kama ingekuwa ni soka, basi yeye ni Mbwana Samatta yani yupo kwenye level hizo.

No comments