Penzi la Bibi wa Miaka 60 Laua Kijana wa Miaka 23
KIJANA mwenye umri wa miaka 23 na mpenzi wake, bibi mwenye umri wa miaka 60 , wakazi wa kijiji cha Tentula, Kata ya Ikozi wilayani Sumbawanga, wanashikiliwa na polisi wakihutumiwa kumshambulia na kumuua kikatili jirani yao aitwae Desder Justino (23) kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Inaelezwa kuwa, Justino pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bibi huyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mauaji hayo yalitokea Desemba 21 mwaka huu saa nne asubuhi katika nyumba ya mwanamke huyo iliyopo kijijini Tentula.
Taarifa kutoka kijijini humo zinadai kuwa, mwanamke huyo licha ya umri wake kuwa mkubwa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana hao wawili wa rika moja.
Kamanda Kyando hakuwa tayari kutaja majina ya wapenzi hao ambao ni watuhumiwa wa mauaji kwa sababu za uchunguzi.
Lakini alisema mwanaume ana umri wa miaka 23 huku mpenzi wake ana umri wa miaka 60. Akielezea zaidi, Kamanda Kyando alisema siku ya tukio Justino alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi na kumkuta kijana mwingine (mtuhumiwa), na hapo ndipo ugomvi ukaibuka baina ya vijana hao.Alisema Justino alijeruwa kichwani.
“Wawili hao yaani wapenzi hao (mwanamke na mwanaume) walimshambulia Justino (Desder) kwa kumpiga kichwani na kitu chenye ncha kali na kumjeruhi vibaya na alikufa akiwa anatibiwa hospitalini,”alisema Kamanda Kyando na kuongeza kuwa, watuhumiwa hao wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani uchunguzi wa awali utakapokamilika.
Post a Comment