Mbunge Sugu anusurika ajali, mtoto afariki kwenye ajali hiyo
Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV leo December 17 2016 zinasema kuwa mbunge wa Mbeya mjini ‘CHADEMA’, Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto ’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.
Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi ‘sugu’.
Post a Comment