GGM yajenga Jengo la Upasuaji lenye thamani ya milioni 335 Wilayani Chato
HABARI NA :GEITA INFO
Mgodi wa Dhahabu wa Geita unajenga jengo la upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Chato lenye thamani ya shilingi milioni 335 ambalo litakua na uwezo wa kufanya upasuaji kwa watu watatu kwa wakati mmoja.
Kwa sasa Hospitali ya Wilaya ya Chato ina chumba cha upasuaji kinachoweza kupasua mtu mmoja tu hali ambayo inahatarisha maisha ya wenye uhitaji huo hasa inapotokea kuwa watu zaidi ya mmoja wanatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa wakati mmoja.
Post a Comment