Diamond Atikisa Australia....Wimbo Wake Wavunja Rekodi ya Mwaka.
Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake.
Siku moja baada ya DW kuitaja ngoma aliyoshirikishwa na marehemu Papa Wemba, Chacun Pour Soi kuwa imefunga mwaka kwa kuwa namba moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kidogoaliyowashirikisha P-Square nayo imefunga mwaka kwa kishindo.
Wimbo huo umekuwa wimbo wa mwaka katika kituo cha redio cha Radio Afro cha Australia, baada ya kuzishinda nyimbo za magwiji wengi wa Afrika wakiwemo Wizkid, Davido, Tiwa Savage na wengine kibao.
Diamond ameshukuru kwa nafasi hiyo kwa kusema, “Thank you AUSTRALIA thank you RADIO AFRO…. KIDOGO ft P -SQUARE Song of the Year #RADIOAFRO.”
Post a Comment