Utafiti umetaja nchi za Afrika ambazo ni hatari zaidi kutembea na kuendesha baiskeli
Taarifa hii imeripotiwa na BBC ambapo imesema kuwa Shirika la mazingira la Umoja wa mataifa UNEP limesema kati ya watu milioni 1.3 wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, 49% ni watu wanaotembea, waendesha baiskeli na pikipiki.
Utafiti wa umoja wa mataifa kuhusu ajali za barabarani umezitaja nchi za Malawi, Kenya na Afrika kusini kuwa nchi hatari zaidi kutembea kwa miguu na kuendesha baiskeli,
Takwimu za watu waliokufa wakitembea au wanapoendesha baiskeli katika ajali za barabarani:
- Malawi: 49% wanaotembea, 14-17% wanaoendesha baiskeli
- Kenya: 47% wanaotembea, 14% wanaoendesha baiskeli
- Afrika kusini: 50% wanaotembea, 3% wanaoendesha baiskeli.
UNEP imesema uwekezaji wa dharura unahitajika kuimarisha miundombinu ya kutembea na kuendesha baiskeli ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.
Ripoti ya utafiti huo wa UNEP iliyopewa jina ‘Global Outlook on Walking and Cycling’, inaeleza kuwa ukosefu wa uwekezaji katika kuhakikisha watu wanatembea na kuendesha baiskeli salama ndiyo unaochangia vifo vya mamilioni ya watu na kupuuza nafasi nzuri ya kuchangia katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Post a Comment